Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018. BONYEZA HAPA KWENDA KWENYE MATOKEO! Akizungumza na vyombo vya habari Dkt. Msonde alisema ufaulu kwa ujumla umeongezeka kutoka asilimia 96.06 ya mwaka jana na kuwa asilimia 97.12 mwaka huu, ingawa ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka kulinganisha na masomo ya biashara na sanaa. Vile vile ufaulu katika madaraja ya I, II na III umeongezeka ukilinganisha na mwaka jana. Ufaulu wa madaraja haya umeongezeka kwa asilimia 1.80 kutoka asilimia 93.72 ya mwaka jana na kuwa asilimia 95.52 kwa mwaka huu. Shule kumi zilizofaulu vizuri kitaifa ni kama ifuatavyo Na Shule Idadi ya watahiniwa Mkoa 1 Kibaha 121 Pwani 2 Kisimiri 68 Arusha 3 Kemebos 32 Kagera 4 Mzumbe 121 Morogoro 5 Feza Boys 93 Dar es salaam 6 Marian Boys 78 Pwani 7 Ahmes 76 Pwani 8 St Mary's Mazinde Juu 189 Tanga 9 Marian Girls 71 Pwani 10 Feza Girls 75 Dar es salaam BONY...