Skip to main content

Matokeo ya kidato cha sita 2018 haya hapa!

Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

BONYEZA HAPA KWENDA KWENYE MATOKEO!

Akizungumza na vyombo vya habari Dkt. Msonde alisema ufaulu kwa ujumla umeongezeka kutoka asilimia 96.06 ya mwaka jana na kuwa asilimia 97.12 mwaka huu, ingawa ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka kulinganisha na masomo ya biashara na sanaa.

Vile vile ufaulu katika madaraja ya I, II na III umeongezeka ukilinganisha na mwaka jana. Ufaulu wa madaraja haya umeongezeka kwa asilimia 1.80 kutoka asilimia 93.72 ya mwaka jana na kuwa asilimia 95.52 kwa mwaka huu.

Shule kumi zilizofaulu vizuri kitaifa ni kama ifuatavyo

Na Shule Idadi ya watahiniwa Mkoa
1 Kibaha 121 Pwani
2 Kisimiri 68 Arusha
3 Kemebos 32 Kagera
4 Mzumbe 121 Morogoro
5 Feza Boys 93 Dar es salaam
6 Marian Boys 78 Pwani
7 Ahmes 76 Pwani
8 St Mary's Mazinde Juu 189 Tanga
9 Marian Girls 71 Pwani
10 Feza Girls 75 Dar es salaam

BONYEZA HAPA KWENDA KWENYE MATOKEO!

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...