Skip to main content

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators).
Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani.
Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ).

Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa.

Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana
= == x == y x ni sawa na y
!= x != y x sio sawa na y

Jedwali ilifuatalo linaonesha alama za uhusiano

Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana
> > x > y x ni kubwa kuliko y
< < x < y x ni ndogo kuliko y
>= x >= y x ni kubwa kuliko au sawa na y
<= x <= y x ni ndogo kuliko au sawa na y

Katika programu ili kucheki sharti (condition) flani kama tulivyosema hapo juu tunatumia if(kama) statement. if inaiambia programu iangalie sharti liloandikwa kwenye if, kama sharti ni kweli(mfano grade > 80), programu itaingia katika body(mwili) ya if. Kama sharti sio kweli basi programu itaendelea na kuruka body ya if.

Muundo wa if

if ( masharti )
{ /* mwanzo wa if */

/* statement zingine za programu */

} /* mwisho wa if */

kama tunavyoona, if inakua na masharti ndani ya mabano, inaweza kuwa sharti moja au zaidi. Curly braces ({ na }) zinawakilisha body ya if. Masharti ya if yanatengenezwa kwa kutumia alama za usawa au alama za uhusiano, kama tulivyoona kwenye mfano wa grade za wanafunzi. katika C, jibu la sharti ni true(kweli) au false(si kweli).

Mfano wa programu ya grade kwa kutumia if

if ( grade > 80 )
{
 printf("Grade ni A!");
}

KUMBUKA:
Katika C, false(si kweli) ni namba sifuri na true(kweli) ni namba yoyote ambayo sio sifuri.

Kwa mfano,

if ( 0 ) => itakua false, kwa hiyo programu itaruka body ya if na kuendelea mbele
if ( 1 ) => itakua true, kwa hiyo programu itaingia ndani ya body ya if
if ( -1 ) => itakua true, kwa hiyo programu itaingia ndani ya body ya if

Programu rahisi ya C: Programu ya kujua grade ya mwanafunzi ni A au sio A
Ili kuelewa zaidi matumizi ya if na alama za usawa na uhusiano, tutatengeneza programu ya kujua kama grade ya mwanafunzi ni A au sio A. Katika programu hii, mtumiaji ataingiza marks za mwanafunzi, kisha programu itaamua kama marks zilizoingizwa ni A au sio A na kuprint jibu katika screen.

Programu ifuatayo inaonyesha jinsi ya kujua grade ni A au sio A

#include <stdio.h>

/* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */
int main(void)
{
    int grade; /* Tutahifadhi marks(alama) za mwanafunzi hapa */
    
    printf("Andika marks za mwanafunzi\n"); /* julisha kuwa namba inatakiwa kuingizwa */
    scanf("%d", &grade); /* soma integer(tarakimu), kisha ihifadhi kwenye variable grade */
    
    /* Cheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 */
    if ( grade >= 80)
    {
        printf("Grade ni A!\n");
    }

    /* Cheki kama grade ni ndogo kuliko 80 */
    if ( grade < 80)
    {
        printf("Grade sio A!\n");
    }
    
    return 0; /* Programu imemalizika bila tatizo */
    
} /* Mwisho wa main */

Output 1:

Andika marks za mwanafunzi
95
Grade ni A!

Output 2:

Andika marks za mwanafunzi
78
Grade sio A!

printf(“Andika marks za mwanafunzi\n”); /* julisha kuwa namba inatakiwa kuingizwa */
Hii inaiambia printf iandike “Andika marks za mwanafunzi”, kisha cursor ipelekwe kwenye mstari unaofuata.

scanf("%d", &grade); /* soma integer(tarakimu), kisha ihifadhi kwenye variable grade */
Hii inaiambia scanf isome tarakimu (integer) kutoka kwa keyboard kisha iihifadhi katika variable grade.

if ( grade >= 80)
Hapa programu inacheki kama grade ambayo imeingizwa ni kubwa kuliko au sawa na 80.

Katika “Output 1”, mtumiaji aliingiza 95 kwenye grade, hivyo sharti likawa ( 95 >= 80) ambayo ni kweli, kwa hiyo programu ikaingia ndani ya body ya if na kuandika “Grade ni A!” kwenye screen.

Katika “Output 2”, mtumiaji aliingiza 78 kwenye grade, hivyo sharti likawa ( 78 >= 80) ambayo si kweli, kwa hiyo programu iliruka body ya if na kuendelea mbele.

if ( grade < 80)
Hapa programu inacheki kama grade ambayo imeingizwa ni ndogo kuliko 80.

Katika “Output 1”, mtumiaji aliingiza 95 kwenye grade, hivyo sharti likawa ( 95 < 80 ) ambayo si kweli, kwa hiyo programu ikaruka body ya if na kuendelea mbele.

Katika “Output 2”, mtumiaji aliingiza 78 kwenye grade, hivyo sharti likawa ( 78 < 80 ) ambayo ni kweli, kwa hiyo programu ikaingia ndani ya body ya if na kuandika “Grade sio A!” kwenye screen.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi