Skip to main content

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi?

Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet.

Kwa njia ya mtandao


Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo.

http://tms.tpf.go.tz

Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako.

Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako.

Kwa njia ya simu

Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75# , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Comments

  1. T773 BWX NAOMBA MSAA NIMEBIWA NADAIWA LAKISITAAA NA MTANDAO UNASUMBUA MSAA WENU NIMEN'GOLEWA PLATI NAMBA ZA GARI LANGUUU 0762768915 NAMBA YANGUUU

    ReplyDelete
  2. T773 BWX NAOMBA MSAA NIMEBIWA NADAIWA LAKISITAAA NA MTANDAO UNASUMBUA MSAA WENU NIMEN'GOLEWA PLATI NAMBA ZA GARI LANGUUU 0762768915 NAMBA YANGUUU

    ReplyDelete
  3. Naomba msaada wa kujua leseni namba 4000336475 Jina ni Anthony James kama inadaiwa maana sijaandikiwa faini popote lakini naambiwa inadaiwa 120,000/=

    ReplyDelete
  4. Jamani trafiki kachukua leseni yangu kaipiga picha na namba ya gari kaipiga picha alafu kaniamvia niende kumbe kesho yake kaniandikia faini mbili je Ni haki kisheria?

    ReplyDelete
  5. Naomba nijue Kama nadaiwa leseni namba no 4004239905


    ReplyDelete
  6. Naombeni no za kumbukumbuk t642dul mtandao unasumbua na kesh vyeti vinazidi dah

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi