Skip to main content

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia.

Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza.

Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri.

Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii hutokea mara chache, kama vile ukitaka kutype namba zilizopo kwenye number pad.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kutype

  1. Hakikisha umekaa vizuri na mikono yako ipo comfortable, hii itarahisisha kusogeza vidole na mikono kirahisi pindi inapohitajika.
  2. Vidole vyako vina sehemu maalumu ya kukaa ambayo ni ASDF kwa mkono wa kushoto na JKL; kwa mkono wa kulia. Vidole gumba unaviacha hauviweki kwenye hizi herufi. Huu mstari huitwa HOME ROW, yaani hapa ndio NYUMBANI ikitokea umehamisha kidole kwenda kubonyeza sehemu ingine inabidi ukirudishe NYUMBANI baada ya kumaliza.
  3. Kwenye herufi F na J utaona kuna kama kauvimbe fulani, hii inasaidia kuweza kurudi kwenye HOME ROW bila kuangalia keyboard.
  4. Usiangalie keyboard wakati wa kuandika, kumbuka lengo ni mazoezi ya vidole ili ubongo wako uzoee kufanya hivyo.
  5. Kila kidole kina vitufe ambavyo kinaruhusiwa kubonyeza, hivyo usitumie kidole tofauti. Pia kumbuka kurudi kwenye HOME ROW baada ya kubonyeza kitufe fulani.

Software au Programu za kujifunzia kutype

Tumeona namna kutype bila kuangalia kunavyofanya kazi, lakini ili kufanya mazoezi vizuri kuna programu nyingi za kompyuta zinazofundisha kutype.

Uzuri wa programu hizi zinapima spidi yako na uwezo wako wa kutype bila kukosea kadri unavyofanya mazoezi.

Pia programu hizi zinakua zinafundisha kwa mtindo wa games, labda ukitype haraka unapata marks fulani na kadhalika. Programu mojawapo yenye mtindo huu ni ile ya Typing Master.

Baadhi ya programu za kujifunzia kutype

  1. Typing Master (Maarufu)
  2. Kiran’s Typing Tutor (BURE)
Zingatia:

Ni bora kutype taratibu bila kukosea kuliko kutype haraka na makosa, kwa hiyo wakati unajifunza lengo kubwa jifunze namna ya kutumia vidole vyako na kuandika bila kukosea. Spidi ya kutype itakuja taratibu ukishaelewa matumizi sahihi ya vidole.

Hitimisho

Ni vizuri kutumia programu kujifunzia kutype, vile vile ni vyema kujitengea muda kila siku hata kama ni nusu saa kwa siku, kwani kutype ni kama mazoezi ukiyaacha unasahau, ukiyafanya kila mara unakua mjuzi zaidi.

Comments

  1. It is useful to me, and I wish if I would get your contacts.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...