Skip to main content

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali.

File la zip ni nini?

File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma.

Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text).

Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size.

Naandaa vipi file la zip?

Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zip unafanana na ule wakutengeneza folder katika kompyuta yako.

Kwanza right-click sehemu ambayo haina file kama kwenye desktop au sehemu nyingine yoyote katika kompyuta yako. Nenda kwenye "New" kisha chagua "Compressed (zipped) Folder".
Sasa unaweza kuchagua mafile yako yote na kuyadrag kwenye zip folder. Mafile yako yatakopiwa kwenye zip file bila kuyafuta kwenye sehemu yalipokuwa.

Nafungua vipi file la zip?

Ili kufungua file la zip, right-click kwenye hilo file kisha chagua "Extract All".
Itakuletea window ya kuchagua sehemu ya kufungulia hilo file. Kwa kawaida zip file linafunguliwa sehemu ile ile ambapo original file lipo. Bonyeza "Extract" utaona folder mpya limetengenezwa ambalo ndani yake kuna mafile yako.

Naweka vipi password kwenye file la zip?

Ili kuweka neno la siri(password) katika file lako utahitaji software ya ziada kama vile 7-Zip na zingine kwani kwa sasa windows haina uwezo huu.

Kwanza kabisa chagua folder lako lenye mafile, right-click na uchague "7-Zip", kisha bonyeza "Add to archive"
Itakuja window nyingine yakuingiza password na kuchagua aina ya encryption.
Hakikisha kwenye "Archive format" umechagua zip. kisha jaza password yako na chagua "AES-256" kwenye "Encryption method"

AES-256 ni bora kuliko ZipCrypto kwani si rahisi kuhackiwa kama ilivyo ZipCrypto, hivyo ni vizuri uchague AES-256. ZipCrypto pamoja si bora kiusalama inafanya kazi katika kompyuta nyingi zaidi kuliko AES-256.

Jinsi ya kuvunja file kubwa la zip kuwa vipande vidogo vidogo

Kabla hatujaenda kwenye namna ya kuvunja file kubwa la zip, kwanza tufahamu ni kwa nini uvunje file hilo?

Tuchukulie una file lenye size ya 2GB (2048MB) na unataka kuliweka kwenye CD ambayo uwezo wake ni 700MB. Unaweza kulivunja file la 2GB mara tatu, kisha kila kipande kitatosha kwenye CD yake, hivyo utahitaji CD tatu kuhifadhi file hili.

Sasa tuone ni namna gani unaweza kuvunja file la zip. Ili kuvunja file la zip utahitaji software ya ziada katika kompyuta yako kwa wale wa windows, 7-Zip ni nzuri kwa kazi hii, kwani inavunja pia itakusaidia kuyasoma haya mafile uliyovunja.
7-Zip inakupa uwezo wa kuchagua size ambazo unataka kuvunja kutegemeana na mahitaji yako. kwa mfano wetu wa CD ya 700MB tutachagaua 700MB - CD, lakini pia inakupa uwezo wa kuchagua size yoyote unayotaka wewe.

Ili kufungua hivi vipande vya file, inabidi vyote viwe kwenye sehemu moja. Ukisha hakikisha vipande vyote vipo sehemu moja, fungua file la kwanza, 7-Zip au software nyingine unayotumia itaunganisha vipande vyote kisha kukutolea yaliyomo kwenye zip file lako.

Jinsi ya kupunguza ukubwa wa file la zip

Wakati wakutengeneza zip file 7-Zip inakupa uwezo wa kuchagua kiwango cha kupunguza ukubwa wa file yaani compression level.
Ukichagua Store, mafile yako yatawekwa kwenye kifurushi kimoja bila kupungua size.

Ukichagua chochote zaidi ya "Normal" utapata kifurushi kidogo zaidi lakini pia itachukua muda zaidi kutengeneza kifurushi, hivyo ni vyema uangalie uwezo wa kompyuta yako pia.

Vile vile kama unataka file dogo zaidi, kwenye "Archive format" chagua "7z". 7z ni aina nyingine ya file la kifurushi kama zip isipokuwa lina uwezo mzuri wa kupunguza size. Changamoto ya 7z ni kama unatuma hilo file kwa mtu, atakaelifungua itabidi naye awe na program ya 7-Zip wakati zip file la kawaida mtu anafungua moja kwa moja bila kuinstall programu yoyote katika Microsoft windows za siku hizi.

(BONUS) Aina zingine za mafile ya vifurushi(archive)

Kuna aina nyingine nyingi za mafile ya vifurushi, hapa tuone mafile ambayo huenda haujui kama ni mafile ya vifurushi.

Kama ulikua hujui programu za Android zinakua katika file la .apk . File hili ni kifurushi aina ya zip! Jaribu kulifungua uone vilivyomo ndani!

Kwa wale wanaotumia Debian Systems kama vile Ubuntu watakua wanajua file aina ya .deb . Software za debian huwa zinatumia file hili la .deb kama ilivyo .exe kwenye windows. File hili la .deb ni aina nyingine ya kifurushi cha aina ya .ar .

Kwa wale wanaotumia java, watakua wamekutana na file aina ya .jar . File la .jar ni kifurushi cha zip. Jaribu kwa kufungua file la .jar kwa kutumia programu yoyote ya zip uone vilivyomo ndani!

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii