Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2018

Control structures katika C

Control Structures katika C Katika somo hili tutajifunza vitu au vipande mbali mbali vinavyounda programu kwa ujumla. Kwa kawaida kompyuta inarun programu mstari mmoja baada ya mwingine kwa kufuatana upi umeanza na upi unafuata. Mstari wa kwanza unarun, kisha unaofuatia na kuendelea hadi mwisho wa programu. Ili kuwepo na wigo mpana wa kuunda programu inabidi tuweze kuhama au kuruka mstari mmoja kwenda mwingine kutegemeana na masharti. Hii huwa inaitwa "Transfer of Control". Hapo awali programmers walikuwa wanatumia goto statement, ambayo inaiambia programu iende kwenye mstari fulani kutegemea na sharti fulani. Ilikuja kugundulika kuwa hii goto statement ilisababisha ugumu mkubwa kwa watengenezaji wa programu kwani kwenye programu kubwa ya kiuhalisia unakuta kuna goto nyingi ambapo inafika kipindi inakua vigumu kujua au kukumbuka statement fulani ilikua kwa sababu gani. Katika utafiti uliofanywa na Bohm na Jacopini walifanikiwa kuonesha kuwa programu zinaweza kutenge...