Control Structures katika C
Katika somo hili tutajifunza vitu au vipande mbali mbali vinavyounda programu kwa ujumla.Kwa kawaida kompyuta inarun programu mstari mmoja baada ya mwingine kwa kufuatana upi umeanza na upi unafuata. Mstari wa kwanza unarun, kisha unaofuatia na kuendelea hadi mwisho wa programu.
Ili kuwepo na wigo mpana wa kuunda programu inabidi tuweze kuhama au kuruka mstari mmoja kwenda mwingine kutegemeana na masharti. Hii huwa inaitwa "Transfer of Control".
Hapo awali programmers walikuwa wanatumia goto statement, ambayo inaiambia programu iende kwenye mstari fulani kutegemea na sharti fulani. Ilikuja kugundulika kuwa hii goto statement ilisababisha ugumu mkubwa kwa watengenezaji wa programu kwani kwenye programu kubwa ya kiuhalisia unakuta kuna goto nyingi ambapo inafika kipindi inakua vigumu kujua au kukumbuka statement fulani ilikua kwa sababu gani.
Katika utafiti uliofanywa na Bohm na Jacopini walifanikiwa kuonesha kuwa programu zinaweza kutengenezwa bila kutumia goto statement yoyote. Katika utafiti huu walionesha kuwa programu yoyote inaweza kuandikwa kwa kutumia "Control Structures" tatu tu, ambazo ni "Sequence Structure", "Selection Structure" na "Repetition Structure".
Sequence Structure
Sequence structure tayari ipo katika C, kwani programu zinarun kuanzia mstari wa mwanzo, kisha unaofuata na kuendelea kwa mpangilio wa uandishi. Structure hii tayari ndio C inavyorun haihitaji statement yoyote ya kuandikwa.Selection Structure
C inakupa aina tatu za selection structure, ambazo ni if selection statement, if...else selection statement na switch selection statement. Hizi ni statement ambazo zinakusaidia kuchagua baina ya vitendo tofauti kutokana na masharti.if selection statement yenyewe inachagua au kufanya kitendo kama sharti ni kweli(true) au inaruka hicho kitendo kama sharti si kweli(false). Katika statement hii kitendo ni kimoja ambacho kinafanywa au kurukwa.
if...else selection statement inafanya kitendo kimoja kama sharti ni kweli(true) au kufanya kitendo kingine kama sharti si kweli(false). Katika statement hii vitendo ni viwili, kwa kutumia sharti moja unachagua baina ya vitendo viwili.
switch selection statement yenyewe inafanya kitendo kimoja baina ya vitendo vingine vingi kutegemeana na thamani ya variable fulani. Katika statement hii vitendo ni vingi na masharti ni mengi, kwa hiyo kila sharti litachagua kitendo chake fulani.
Comments
Post a Comment