Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75# , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.