Je unataka kujua namna ya kufanya mahesabu katika programu? Programu yetu ya sasa itaonyesha namna ya kujumlisha namba mbili ambazo mtumiaji atakuwa ameingiza kwa kuandika na keyboard yake. Kama tulivyojifunza hapo awali kuwa stdio.h ni “Standard Input/Output header”, ambalo ni file lenye functions zinazohusiana na input(kuingiza) au output kama vile printf, kwenye somo hili tutajifunza function mpya ya scanf. Kazi ya scanf ni kuchukua/kusoma alichoandika mtumiaji kwa keyboard na kukihifadhi katika kompyuta kwa matumizi ya baadae kwenye programu. Programu ifuatayo inaonyesha kujumlisha tarakimu mbili #include <stdio.h> /* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */ int main(void) { int namba1; /* namba ya kwanza itakayoingizwa */ int namba2; /* namba ya pili itakayoingizwa */ int jumla; /* variable itakayohifadhi jumla */ printf("Andika namba ya kwanza\n"); /* julisha kuwa namba inatakiwa kuingizwa */ scanf("%d"...