Je unataka kujua C ilitokea wapi? na kipindi gani?
Lugha ya kuandikia programu za kompyuta ya C ilianzishwa mnamo mwaka 1970 na mbunifu wake Dennis Ritchie. Aliita C kwa sababu kipindi hicho alikuwa akitumia lugha iitwayo B katika kazi zake, hivyo C ilifuata baada ya B. Mbunifu wa C alichukua mazuri ya B na kuyaweka kwenye C, vile vile akaongeza maboresho ambayo kwenye B yalikuwa ni vikwazo.
C ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kutengenezea OPERATING SYSTEMS kwa kipindi hicho UNIX. Hata mbunifu wa B alipotengeneza B alianza kuitumia kuandikia UNIX OPERATING SYSTEM. C ilikuwa rahisi sana kutumia, hivyo ikaanza kutumika katika matumizi mengine nje ya OPERATING SYSTEMS. Haikuchukua muda mrefu C ikawa lugha maarufu sana duniani kote ya kuandikia programu za kompyuta.
Umaarufu wa C ulichangiwa na urahisi wake, ambapo programmer aliweza kufanya chochote alichotaka kirahisi bila kupitia vikwazo vingi. Vile vile programu za kubadilisha C kwenda kwenye MACHINE CODE yaani COMPILER zilipatikana kirahisi, hivyo mtu yeyote aliweza kuandika C na kutumia C COMPILER ya kompyuta yake kutengeneza programu.

Comments
Post a Comment