Skip to main content

Jinsi ya kujifunza lugha ya kuprogramu ya C

Je unataka kuwa mtaalamu wa kutengeneza programu za kompyuta? unataka kufahamu njia ya kutimiza lengo lako kirahisi?

Waswahili wanasema "Mtaka cha uvunguni sharti ainame" basi ndivyo hivyo hivyo ili kuwa mtaalamu wa kuprogramu inabidi uwe unaandika programu. Ujuzi wowote unaushika vizuri zaidi ukiwa ni mtendaji. Utajifunza mengi sana kwa kuandika programu zaidi ya kusoma C kwenye vitabu na mtandaoni. Hivyo weka bidii kufanya mazoezi tofauti tofauti ya kuprogramu iwe kwenye vitabu au kutengeneza programu ya suluhisho ya matatizo uliyoyaona mtaani, kwenye biashara au sehemu nyingine.

Pia wakati unafanya mazoezi haya jitahidi kufuata miongozo ya kuandika programu nzuri yaani GOOD PROGRAMMING GUIDELINES. Kwenye programu zako hakikisha zinasomeka vizuri kwa maana nafasi kati ya maneno au mistari iwe ya kutosha. Pia jitahidi kuweka maoni (COMMENTS) ili iwe rahisi wewe kuelewa au mtu mwingine kuelewa programu yako. Ni kawaida kwa programmer kusahau sehemu flani ya programu yake ilikuwa inafanya kazi gani baada ya muda mrefu kupita, kuandika maoni kutakusaidia kuielewa programu yako baadae.

Chagua IDE (Integrated Development Environment) yoyote uiweke kwenye kompyuta yako uwe ndio unaitumia kuandikia programu. Kwa sasa kuna IDE nyingi sana za C kwa mfano unaweza kutumia codelite, Dev C++ , Eclipse au Netbeans. Angalia Download Links chini kudownload mojawapo. Kwa anayeanza kuprogramu Dev C++ ni nzuri. Pia codelite inamfaa anayeanza.

Kuna tovuti mtandaoni zinakupa uwezo wa kuandika C na kuCOMPILE na kukupa matokea hapo hapo, mfano mzuri ni https://www.onlinegdb.com/ . Pia kuna applications ambazo unaweza kuweka kwenye simu yako ambazo zina EDITOR na COMPILER tayari, kwa hiyo unaweza kujaribu ulichokiandika kwenye simu.

KUMBUKA: IDE ni programu ambayo tayari ina COMPILER, ASSEMBLER, TEXT EDITOR, DEBUGGER na vitu vingine ambavyo unaweza kuvitumia wakati wa kutengeneza programu.

Download Links:
codelite - https://codelite.org
Dev C++ - https://sourceforge.net/projects/orwelldevcpp/
Eclipse - https://www.eclipse.org
Netbeans - https://netbeans.org

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...