Skip to main content

Jinsi kuprogramu kompyuta kunavyofanya kazi

Je unajiuliza ni namna gani kuprogramu kompyuta kunavyofanya kazi? Leo tutaingia ndani ya kompyuta na kuelewa namna inavyofanya kazi.
  1. MACHINE CODE NA ASSEMBLY LANGUAGE
Kwanza kabisa inabidi tuelewe kwamba kompyuta inaelewa sifuri na moja au ON na OFF pekee, ambazo huitwa BINARY DIGITS. Mfululizo wa hizi binary digits kwa namna ambayo kompyuta inaelewa huitwa MACHINE CODE yaani lugha ya mashine.
Kwa mfano,
Kujumlisha kunaweza kuwakilishwa na 1010
kutoa kukawakilishwa na 1011
ufuatao ni mfano wa programu katika MACHINE CODE:
0011 1111
1010 0111
1011 0110
... na kuendelea
sasa huu mfululizo wa haya maelezo (INSTRUCTIONS) ndio unaounda programu ya kompyuta. Lakini kuna tatizo moja ni vigumu sana kuandika programu kwa machine code, yaani kwa sifuri na moja. kutokana na ugumu huu lugha nyingine ambayo ni rahisi kwa mwanadamu iliundwa ambayo ni ASSEMBLY LANGUAGE.
Lugha hii inatumia maneno kuwakilisha zile zile binary digits. kwa hivyo badala ya programmer kuandika 1010 anaandika ADD, au badala ya kuandika 1011 anaandika SUB.
ufuatao ni mfano wa programu katika ASSEMBLY:
MOV A,7
ADD A,B
SUB A,B
... na kuendelea
Baada ya ASSEMBLY kuandikwa, ili kompyuta iweze kuelewa inabidi ASSEMBLY CODE ibadilishwe kwenda kwenye MACHINE CODE ambayo kompyuta inaelewa. Ili kubadilisha ASSEMBLY CODE kwenda kwenye MACHINE CODE, programu nyingine iitwayo ASSEMBLER hutumika. Hii inabidilisha maneno yaliyoandikwa na programmer kuyapeleka kwenye mfululizo wa sifuri na moja.
  1. HIGH-LEVEL LANGUAGES
ASSEMBLY ni tafsiri ya MACHINE CODE mstari kwa mstari, baada ya muda kuandika ASSEMBLY pia ikawa ngumu ndipo hapo wahandisi wa kompyuta walipogundua inawezekana kuandika programu katika HIGH-LEVEL ambapo neno moja linaweza kuwakilisha instruction zaidi ya moja kwenye assembly. Ubunifu huu ulizaa HIGH-LEVEL LANGUAGES nyingi zikiwemo COBOL, FORTRAN na PASCAL. C pia ni katika HIGH-LEVEL LANGUAGES.
ufuatao ni mfano wa programu katika C:
printf("HAKUNA MATATA!");
Mstari huu mmoja wa C unaiambia kompyuta iandike “HAKUNA MATATA!” kwenye screen.
Inabidi tukumbuke kuwa lugha asili ya kompyuta ni MACHINE CODE hivyo pamoja na kuandika programu kwa kutumia HIGH-LEVEL LANGUAGE inabidi programu hiyo ibadilishwe kwenda kwenye MACHINE CODE. Ili kubadilisha programu ya C kwenda kwenye MACHINE CODE programu iitwayo COMPILER hutumika.
  1. HITIMISHO
Kwa ufupi haijalishi programu imeandikwa katika lugha gani iwe ASSEMBLY (LOW-LEVEL) au HIGH-LEVEL LANGUAGES kama C ni lazima ibadilishwe kwenda kwenye MACHINE CODE ya kompyuta ili iweze kufanya kazi. Hivyo kila tutakapo andika programu katika C itabidi tuiCOMPILE ili tuweze kuijaribu katika kompyuta.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi...