Skip to main content

Programu rahisi ya C: kuandika maandishi kwenye screen

Je unataka kuona jinsi programu ya C inavyoandikwa? Katika somo hili tutajifunza machache katika C, kadri tunavyoendelea kujifunza ntaongeza vitu mbali mbali kidogo kidogo, ili na wewe uweze kutafuna uliyojifunza!

1. Kuandika maandishi kwenye screen

Programu ifuatayo itakuonyesha namna ya kuandika maandishi kwenye screen
#include <stdio.h>

/* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */
int main(void)
{
    printf("Karibu C Programu!\n");
    
    return 0; /* Programu imemalizika bila tatizo */
    
} /* Mwisho wa main */

Output
Karibu C Programu!

1.0. #include <stdio.h>
Hii inaiambia C Preprocessor kuweka yaliyomo katika file la stdio.h kwenye hii programu. File la stdio.h yaani standard input/output header lina maelezo ambayo yanasaidia COMPILER kucompile programu yako kama umetumia function zilizomo humo. Kwa mfano printf ni moja ya function ambazo zipo kwenye stdio.h, kuna zingine nyingi tutaendelea kujifunza. function ni kipande au sehemu ya programu ambayo inafanya kazi fulani. mfano main() ni function na pia printf() ni function. Kama unataka kutumia function ambayo ipo kwenye file lingine ni lazima uinclude hilo file kwenye programu yako. Katika programu yetu tumetumia printf kwa hiyo ni lazima tuinclude file ambalo lina hiyo function. Ni vizuri kuinclude mafile ambayo utatumia functions kabla haujatumia hizo function, kwa hivyo kwa kawaida mafile yote yanayohitajika yanaincludiwa mwanzoni kabisa mwa programu.

1.1. /* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */
Hii ni comment(MAONI). Tunacomment programu ili kuelezea zaidi sehemu ya programu yetu, hivyo kuzifanya ziwe rahisi kusomeka na sisi au watu wengine. Comment hazifanyi kazi yoyote. Hamna ASSEMBLY CODE yoyote inayotolewa na C COMPILER kutokana na COMMENTS. Zingatia ukiandika comment kwa /* inabidi uifunge kwa */ . Usipoifunga utapata ERROR na programu haitaCOMPILE.

1.2. int main(void)
Hii ni function. Programu za C zinaundwa kwa function moja au zaidi na main ikiwepo mara moja tu. main function ndipo ambapo programu huanzia kufanya kazi yake, hivyo ni lazima kwa programu yoyote. function huwa zinarudisha majibu, kushoto kwa main kuna int, hii inaonyesha kuwa main inarudisha jawabu ambalo ni integer(tarakimu). Kulia kwa main kuna mabano (), katika C mabano yatakujulisha kwamba hii ni function. kati kati ya mabano ndipo input za function zinapoandikwa, void imeandikwa kumaanisha function hii haihitaji input yoyote. Alama “{” inaanzisha body ya function yoyote na alama “}” inafunga body ya function hiyo.

1.3. printf(“Karibu C Programu!\n”);
Hii inaiambia kompyuta iandike kwenye screen maneno yaliyopo kwenye quotation marks(""), ambayo yanaitwa STRING. Huu mstari wote wenye printf na semicolon(;) unaitwa STATEMENT. Statement yoyote katika C ni lazima iishie na semicolon(;). Kwa kawaida printf ikianza kufanya kazi yake itaandika herufi moja moja zilizopo katika input yake, mpaka itakapokutana na \ . Alama ya \ inaiambia printf ifanya kitu flani tofauti na kawaida. Kwa mfano \n inaiambia printf ipeleke cursor kwenye mstari unaofuata (newline). Alama ya \ inaitwa escape character, uwepo wake unaashiria kufanyika kwa kitu tofauti.
Zifuatazo ni alama zingine za ESCAPE CHARACTER
\n - Newline: Inapeleka cursor kwenye mstari unaofuata.
\t - Horizontal Tab: Inapeleka cursor kwenda tab inayofuata. Tab character unaipata ukibonyeza TAB kwenye keyboard yako ya kompyuta.
\a - Alert: inapiga sauti kwenye kompyuta.
\\ - Backslash: Kama unataka alama \ pia iandikwe inabidi uziweke mbili, kwa sababu moja tayari inamaanisha escape character.
\" - Double quotes: Kama unataka kuandika alama " kwenye sentensi.

1.4. return 0; /* Programu imemalizika bila tatizo */
Hii inaiambia function main irudishe jibu la sifuri. main imerudisha sifuri kumaanisha programu imemalizika bila tatizo. function yoyote ikisharudisha jibu ndio unakuwa mwisho wa hiyo function. Tutaelewa zaidi matumizi na umuhimu wa return pindi tutakapojifunza functions. Kwa sasa hakikisha unaiweka mwisho wa main kuepuka errors.


2. Kuandika maandishi kwenye screen: zaidi kuhusu printf

Tumeona namna printf inavyotumika kuandika maandishi kwenye screen, hapa tutajifunza zaidi namna printf inavyofanya kazi yake.
Programu ifuatayo inaonesha jinsi printf inavyofanya kazi
#include <stdio.h>

/* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */
int main(void)
{
    printf("Karibu ");
    printf("C Programu!\n");
    
    return 0; /* Programu imemalizika bila tatizo */
    
} /* Mwisho wa main */

Output
Karibu C Programu!

Kama unavyoona pamoja tumetumia printf mbili maneno yaliyoandikwa kwenye screen ni yale yale kama ya printf moja kwenye mfano wa kwanza. Inabidi tufahamu kwamba printf ikianza kuandika hairuki nafasi wala kuhama mstari mpaka tuiambie kwa kutumia \n . Kwa hiyo printf ya kwanza ilipomaliza kuandika "Karibu ", printf ya pili iliendelea pale pale ya kwanza ilipoishia hivyo kuandika “C Programu!”. Tukiziunganisha kwa pamoja tunapata “Karibu C Programu!”. Tazama vizuri nafasi(space) kwenye neno "Karibu " kwenye printf ya kwanza.

3. Kuandika maandishi kwenye screen: escape character

Programu ifuatayo inaonesha athari ya escape character kwenye printf
#include <stdio.h>

/* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */
int main(void)
{
    printf("Karibu\nC\nProgramu!\n");
    
    return 0; /* Programu imemalizika bila tatizo */
    
} /* Mwisho wa main */

Output
Karibu
C 
Programu!

Kwenye mfano huu pamoja tumetumia printf moja tunaona ya kwamba printf imeandika maneno katika mistari mitatu na si mstari mmoja. Ni muhimu kuelewa printf haihami mstari mpaka tunapoiambia kwa kutumia \n. Hapa kilichotokea ni kwamba printf iliandika “Karibu” kisha ikaona kuna \n ambayo inaiambia iende mstari unaofuata, baada ya hapo ikaandika “C”, kisha ikakutana tena na \n, hivyo ikahamia mstari mwingine, ilipoendelea ikaandika “Programu!”, kisha ikakutana na \n, ikahamia mstari unaofuata.

Comments

  1. The King Casino and Resort
    The king casino and resort features a modern casino https://septcasino.com/review/merit-casino/ with worrione.com everything you'd expect https://deccasino.com/review/merit-casino/ from 바카라 사이트 a classic Vegas Strip casino. The resort features 50000 square feet of Funding: $250 millionDesign: Inspired DesignMasters: Ivan ventureberg.com/ Karaszko

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi...