Skip to main content

Algorithm na Pseudocode

Je unataka kujua mbinu ya kuandika programu iliyo bora? unataka kuwa tofauti na programmer wengine wa kawaida?

Algorithm ni nini?
Algorithm ni MFULULIZO wa hatua zilizo katika MPANGILIO MAALUMU zinazofanikisha kazi fulani.
Mfano unaweza kuwa na kazi ya kuhesabu watu, au kazi ya kuamka asubuhi au kazi ya kula chakula au kazi na kutengeneza juisi.

Katika kazi ya kula chakula, algorithm inaweza kuwa hivi
  1. Pika chakula
  2. Andaa chakula mezani
  3. Nawa mikono
  4. Kula
Na katika kazi ya kutengeneza juisi, mfano juisi ya nanasi, algorithm inaweza kuwa hivi
  1. Osha tunda
  2. Menya nanasi
  3. Kata vipande vidogo vidogo
  4. Weka vipande katika blenda
  5. Ongeza maji na sukari
  6. Saga mchanganyiko katika blenda
Mpangilio katika Algorithm
Katika hatua hizi za algorithm utagundua kwamba tukigeuza hatua tu, tunaweza kuharibu hiyo kazi. Kwa mfano, katika kazi ya kutengeneza juisi ya nanasi, tukihamisha hatua ya kwanza kuwa ya mwisho, tutakuwa tumetengeneza juisi yenye uchafu katika maganda yake. Hivyo basi wakati wa kutengeneza algorithm ya kazi fulani ni vizuri kuelewa hiyo kazi vizuri, kabla ya kubuni algorithm.

Umuhimu wa Algorithm
Algorithm ndio zinazoongeza neno sayansi katika “sayansi ya kompyuta”. Kwa maana, tatizo moja linaweza kuwa na suluhu nyingi tofauti, utajuaje suluhu ipi ni bora? Ndipo hapo uchambuzi wa algorithm kutokana na muda utakaotumika au ukubwa wa memory itakayotumika na kadhalika unapokuwa muhimu. Kama programmer ni muhimu sana kufahamu algorithms kwani itafanya programu zako ziwe zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia muda na memory inayotumika.

Tofauti ya programmer wa kawaida na programmer ambaye ni mtaalamu wa algorithm ni sawa na fundi nyumba wa mtaani na mhandisi wa ujenzi(Civil Engineer). Fundi nyumba wa mtaani anaweza kutengeneza nyumba ya chini vizuri tu, lakini ukimpa kazi ya kukutengenezea jengo la ghorofa kumi hatoweza, kwa sababu hafahamu mahesabu yanayotumika kufanya jengo lisimame imara.

Baadhi ya algorithm ambazo wanasayansi wa kompyuta wamehangaika nazo kwa muda mrefu ni kama Sorting Algorithms(Algorithm za kupanga vitu), Search Algorithms (Algorithm za kutafuta kitu) na zingine nyingi. Kuna Sorting Algorithms zaidi ya 30 katika sayansi ya kompyuta.

Jedwali lifuatalo linaonesha aina zaidi ya 30 za Sorting Algorithms



Programmer mahiri anatumia algorithm ambazo zimeshagunduliwa au anatengeneza algorithm yake kama zilizopo sio bora.

JE WAJUA? 
Neno algorithm limetokana na jina la mgunduzi wa Algebra yaani Al-Khwarizmi, ambaye walatini walimwita Algoritmi.

Pseudocode ni nini?
Pseudocode ni lugha isiyo rasmi, iliyobuniwa kwa lengo la kurahisisha utengenezaji wa Algorithm. Lugha hii inatumia maneno ya kawaida ya kimazungumzo. Lengo la lugha hii ni kusaidia kuwaza algorithm vizuri kabla haijabadilishwa kuwa programu ya kompyuta.

Ufuatao ni mfano wa pseudocode

if grade ya mwanafunzi ni kubwa kuliko au sawa na 80
    Andika “Grade ni A!”

Kama tunavyoona pseudocode yetu imetumia neno if ambalo lipo katika C, lakini maneno mengine ni maneno ya kawaida ya lugha ya mazungumzo. Pseudocode hii inasaidia kuwa na picha kamili ya namna programu itakavyofanya kazi kabla ya kuiandika.

Ni muhimu kutengeneza picha kamili kichwani ya namna programu itakavyofanya kazi kabla ya kuandika programu yoyote. Hii inasaidia kugundua errors(makosa) za kilogik kabla programu haijaandikwa.

JE WAJUA? 
Pseudocode imeundwa na neno pseudo na code. Neno Pseudo lina maana ya inayofanana(LIKE), kwa hiyo pseudocode maana yake ni “Inayofanana na code”

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi