Skip to main content

Arithmetic katika C

Ni kawaida katika programu kutaka kutumia mlinganyo(equation) au kanuni(formula) flani katika programu yako. Kwa mfano unaweza kuandika programu ya kukokotoa eneo la duara, katika programu hii itabidi uandike kanuni ya eneo la duara, hivyo ni muhimu kufahamu alama tofauti za hesabu zinavyoweza kuandikwa katika programu zetu za C.

Jedwali lifuatalo linaonyesha alama katika C na katika aljebra
Alama Aljebra C
Kujumlisha a + b a + b
Kutoa y - x y - x
Kuzidisha ab a * b
Kugawanya x / y au x ÷ y x / y
Baki(Remainder) a mod b a % b

Katika jedwali hili utagundua kwamba alama nyingi za kihesabu zinafanana na zile za C, isipokuwa alama mbili za kuzidisha na baki.
Kuzidisha katika C kunawakilishwa na alama ya asterisk(*), katika hesabu tukiandika ab, inamaanisha a zidisha na b, lakini katika C tukiandika ab inamaanisha jina la variable ab, hivyo ili kuondoa mgongano wa maana, alama ya asterisk(*) hutumika.
Alama ya asilimia(%) inawakilisha baki au salio baada ya kugawanya tarakimu. kwa mfano 5 / 2, inaingia mara 2 na kubaki 1. Hii 1 ndio inayoitwa baki, tutaona matumizi wa baki baadae katika programu zetu.
Kwa mfano,
8 % 3 = 2 (inaingia mara 2, baki 2)
17 % 9 = 8 (inaingia mara 1, baki 8)
103 % 5 = 3 (inaingia mara 20, baki 3)

N.B
Katika C, milinganyo au kanunu zinaandikwa katika mstari mmoja, tofauti na hesabu ambapo tunaweza kuandika sehemu(fraction) , juu na chini. kwa mfano (a + b). Katika C itabidi kubadilisha sehemu hii iwe (a + b) / c

Mpangilio wa kukokotoa - Order of operations
Kama ilivyo kwenye hesabu, kuna mpangilio sahihi wa kukokotoa mlinganyo flani maarufu kama MAGAZIJUTO(BODMAS) hivyo hivyo katika C kuna mpangilio maalum wa ukokotoaji.
Kwa mfano,
2 * 4 + 1 = 9 (kuzidisha kunaanza kabla ya kujumlisha)
15 / 5 - 2 = 1 (kugawanya kunaanza kabla ya kutoa)

Mpangilio wa kokotoa ni kama ifuatavyo
MABANO => GAWANYA => ZIDISHA => BAKI => JUMLISHA => TOA

Utagundua kwamba mpangilio ni ule ule wa katika hesabu, ila BAKI imeongezeka. Katika kompyuta kuna hesabu za ziada kama baki (remainder au modulus), bit shifting ambazo zinaongezeka katika mpangilio wa ukokotoaji. Kwa sasa tufahamu hizi, tutajifunza zingine pindi tutakapo kutana nazo.

Matumizi ya Mabano
Ni vizuri kutumia mabano katika formula zetu ili mpangilio wa kukokotoa uwe rahisi kuonekana, pia inarahisisha kusomeka au kueleweka kwa programu zetu.
kwa mfano,
2 * 4 + 1 = 9 (ni vizuri kuandika (2 * 4) + 1 )
15 / 5 - 2 = 1 (ni vizuri kuandika (15 / 5) - 2 )
150 / 5 * 2 = 60 (ni vizuri kuandika (150 / 5) * 2 )

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...