Skip to main content

Jinsi ya kutafuta scholarship

Je unataka kusoma nchi za nje kwa scholarship? Katika makala hii tutaona njia mbali mbali za kutafuta scholarship.

Mtandaoni
Dunia imebadilika tunaweza kupata taarifa mbali mbali kwenye simu zetu za viganjani au kompyuta, vile vile taarifa za scholarship zinapatikana kwa wingi kwenye mtandao.

Unaweza kutumia google.com kutafuta scholarship zozote unazotaka kwa nchi yoyote duniani. Muhimu ni kuwa specific na unachotaka. Kwa mfano kama unataka kwenda USA ni vizuri ukasearch “scholarships in USA for international students” na sio “scholarships”. Kama matokea yatakayokuja ni machache unaweza kupunguza uspecific wako kidogo. Kwa ufupi inabidi uwe mjanja wa kutumia google.

Vile vile vyuo vikuu vingine huwa vinatoa scholarship kwa wanafunzi wakigeni, hivyo ni vizuri kutembelea tovuti za vyuo hivyo. Mfano vyuo vikuu vingi vya marekani huwa vinatoa scholarships kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya SAT (kwa undergraduate).

Pia kuna tovuti mbali mbali zinazoweka listi ya scholarship tofauti, unaweza kuzipata hizi tovuti kupitia google. Mfano wa tovuti hizo ni
scholars4dev.com

Ubalozini
Sehemu nyingine ambayo unaweza kupata scholarship ni ubalozini. Kama unatafuta scholarship za kwenda Canada ni vizuri ukaenda ubalozi wa Canada na kuulizia. Pia balozi zingine hubandika matangazo ya scholarship nje au ndani ya ubalozi. Baadhi ya scholarship ambazo zimekua zikipitia ubalozini ni kama scholarship za polland, scholarship za serikali ya japan na kadhalika.

Wizara ya Elimu
Sehemu nyingine ambayo scholarships hupitia ni wizara ya elimu. Ni vizuri kutembelea wizara hii na kusoma matangazo mbali mbali yaliyobandikwa. Mfano scholarship za Urusi niliziona pale wizarani miaka ya zamani kidogo.

Vyuo vikuu
Vyuo vikuu pia ni katika sehemu ambazo schokarships za nje hupatikana. Kwa mfano Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwani mara nyingi vyuo huwa vina mahusiano mazuri na vyuo vingine vya nje. BONYEZA HAPA kuona scholarship zilizopitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Semina za vyuo vya nje
Kuna wakati vyuo vya nje kama vya Malaysia, Uingereza na Marekani huwa vinaandaa semina nchini Tanzania. Mara nyingi hizi semina zinafanyika maeneo ya Posta.

Katika vyuo vinavyoleta wawakilishi wao kwenye semina vingine huwa vinatoa scholarships.

Pamoja na scholarship, semina hizi zinasaidia kupata ufahamu juu ya maisha kwenye hiyo nchi na kwenye hicho chuo kwa ujumla.

Vyanzo vingine
Kuna scholarship nyingine huzipati kwa njia tulizojadili, hivyo ni vizuri kuuliza watu waliopita. Kwani kuna scholarship kama zile zinatolewa na makampuni binafsi au foundations ambazo unaweza usizikute mtandaoni wala mahali pengine ila kwa kusikia tu kwa watu wengine.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...