Skip to main content

Kuwa mwalimu wa kiingereza na TEFL

Je unataka kuwa mwalimu wa kiingereza anayetambulika katika nchi nyingi? Au wewe si mwalimu lakini ni mjuzi wa kiingereza na unataka kupata kazi ya ualimu kirahisi? Katika makala hii tutaona mtihani wa TEFL na umuhimu wake.

TEFL kwa kirefu ni Teaching English as a Foreign Language. TEFL ni kwa ajili ya kifundisha kiingereza kwa wanafunzi ambao lugha yao ya asili sio kiingereza. Kwa hiyo TEFL inatumika zaidi katika nchi ambazo haziongei kiingereza kama Spain, Uturuki, China na kadhalika. Pia TEFL hutumika katika nchi zinazoongea kiingereza ili kufundishia kiingereza wahamiaji katika nchi hizo.

Huu ni mtihani ambao ukishafaulu na kupata cheti utakuwezesha kufundisha kiingereza katika shule mbali mbali duniani kote. Ni mtihani wa kimataifa, kwa hiyo unatambulika nchi nyingi.

Vile vile vituo vya kufanyia mtihani huwa vinasaidia kupata kazi katika nchi mbalimbali. Kwa mfano seriousteachers.com wao huwa wanapata kazi nyingi kutoka kwa waajiri wanaohitaji walimu wa TEFL, nao huzisambaza hizi nafasi za kazi kwa wanafunzi au wahitimu wake.

Kuna level mbili tofauti katika mtihani huu ambazo ni certificate na diploma. Bei ya mtihani inatofautiana kulingana na level unayohitaji.

Umuhimu wa TEFL
  • Mtihani huu utakusaidia kupata kazi nchi nyingine
  • Kama wewe ni mwanafunzi katika nchi isiyozungumza kiingereza, unaweza ukatumia mtihani huu kupata ajira. ( Fanya utafiti kama TEFL ni maarufu kwenye hiyo nchi )
Kwa mfano kuna rafiki zangu walikua uturuki walifanya mtihani huu, vyeti walivyovipata viliwasaidia kusoma masomo yao ya juu ya chuo na huku wakijipatia kipato kupitia kazi ya kufundisha kiingereza.

Nafanyaje huu mtihani?
Mtihani huu unafanyika mtandaoni. Ukishajisaji na kulipa ada ya mtihani unapata mfululizo wa masomo ambayo utayachukua na kuyafanyia mtihani. Baada ya kufaulu masomo haya kwa alama zinazotakiwa utapata cheti ambacho utatumiwa mahali utakapopataja.

Kama utaamua kutumia tovuti ya seriousteachers.com tumia link ifuatayo
https://www.seriousteachers.com/TEFL/

Mitihani mingine inayofanana na huu ni TESOL.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...