Skip to main content

Scholarship za uturuki

Je unataka kwenda kusoma nchi za nje hususani uturuki? Makala hii itakuonesha scholarship mbali mbali zinazopatikana nchini uturuki katika ngazi tofauti za elimu, kuanzia High school, undergraduate na kuendelea. Zifuatazo ni scholarship tofauti tofauti za uturuki na utaratibu wake wa kuapply.


Scholarship za serikali ya uturuki
Serikali ya uturuki huwa inatoa scholarship kwa wanafunzi wa nchi mbali mbali kwenda kusoma nchini uturuki katika ngazi tofauti za elimu kuanzia undergraduate mpaka PHD. Pia scholarship hii ni kwa ajili ya masomo yote sio udaktari na uhandisi pekee, kwa hiyo watu wa vitengo vingine wanaweza kuapply kama wahasibu na kadhalika. Application zinafanyika mtandaoni kupitia link ifuatayo.
https://www.turkiyeburslari.gov.tr/en/english-home/

Scholarship za IDB
Scholarship za IDB yani Islamic Development Bank zinatolewa kwa ajili ya wanafunzi wa ngazi mbali mbali kuanzia undergraduate na kuendelea. Scholarship hizi ni kwa ajili ya waislamu. Utaratibu wa kuapply ni kupitia ofisi zao katika nchi husika, hivyo ni vyema kutembelea ofisi au wawakilishi wa IDB katika nchi yako. Tembelea tovuti ya IDB kupata baadhi ya taarifa, japo ni vyema kwenda ofisini kwao.
isdb.org

TUBITAK scholarship
TUBITAK kwa kirefu ni “Türkiye Bilimsel ve Teknolojik Araştırma Kurumu” inayomaanisha “Scientific and Technological Research Council of Turkey”. Hichi ni chombo cha serikali ya uturuki kinachojihusisha na utafiti wa kisayansi na teknolojia. Ili kuendeleza sayansi na teknolojia huwa kinatoa scholarship za ngazi ya masters na kuendelea. Kinatoa scholarship kadhaa kwa wanafunzi wakigeni waliojikita kwenye masomo ya sayansi na teknolojia. Application zinafanyika mtandaoni kupitia link ifuatayo
https://e-bideb.tubitak.gov.tr/giris.htm?language=en

Kwa wanafunzi wa kigeni, scholarship hii imefutwa ( Source - Tubitak )

Turkiye Diyanet Vakfi
Hii ni “Turkish Religious Foundation” ambayo ni foundation ya kidini nchini uturuki. Foundation hii inatoa scholarship kwa masomo ya dini ya kiislamu nchini uturuki. Scholarship zinaanzia ngazi ya High School (A Level) mpaka undergraduate. Applications zinafanyika mtandaoni kupitia link ifuatayo
http://burs.tdv.org

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi...