Skip to main content

Ujue ujanja wa “Fikiria Namba” kihesabu

Je unataka kuwa mjanja wa kusoma fikra za watu? Hapa tutaona namna ya kutumia hesabu kiujanja zaidi.

Ni jambo ambalo watu wengi hawalijui hivyo kuwa rahisi kudanganywa na watu wanaojifanya wanasoma akili za watu.

Ujanja wa variable mbili( Ujanja wa 10x + y)

Katika mfano huu ili usiwe kihesabu zaidi na rahisi kwa kila mtu kuelewa ntatoa mfano wa namna inavyotumika kisha ntawaonyesha kihesabu wewe unavyoweza kufanya na pia kutengeneza mlinganyo wako mwenyewe.

Mfano mtu anaweza kuja akakuambia leo ntakutajia kwenu mpo wangapi, watoto wa kiume ni wangapi na wakike ni wangapi. Ataanza kukuambia chukua idadi ya watoto wa kiume zidisha kwa mbili, kisha jibu jumlisha na tatu, jibu lake zidisha na tano, kisha jumlisha idadi ya watoto wa kike, kisha toa 15 katika jibu. Baada ya hapo atakuuliza jibu ni ngapi. Ukimpa jibu tuseme 23, atakuambia mpo watoto watano, wakiume wawili na wakike watatu. Hapo utaona jamaa bonge la superhero!!

Ngoja tuone namna yakufanya huu ujanja kihesabu

Tuchukulie ifuatavyo:

x= watoto wa kiume
y= watoto wa kike
*= alama ya kuzidisha

Mlinganyo ambao jamaa anatuambia ni huu hapa
(x * 2 + 3 )* 5 + y - 15

Ukiurahisisha unakua
10x + y

Kama y ni ndogo kuliko kumi, hata ufanye vipi idadi ya watoto wa kike itakua kwenye mamoja(yaani 3 kwenye 23)

Na kama x ni ndogo kuliko kumi pia, basi idadi ya watoto wa kiume itakua kwenye makumi(yaani 2 kwenye 23)

Ukishajua watoto wa kike na wa kiume utajumlisha tu idadi yake na kutoa jibu.

Tuone mifano zaidi:
Jibu 14 ( wakiume=1 , wakike=4)
Jibu 32 ( wakiume=3, wakike=2)
Jibu 47 ( wakiume=4, wakike=7)
Jibu 51 ( wakiume=5, wakike=1)
Jibu 63 ( wakiume=6, wakike=3)

Changamoto ili huu ujanja usifanye kazi
Kama tulivyoona hapo juu y ikizidi kumi tayari hesabu inaharibika, kwa hiyo jifanye watoto wa kike wapo zaidi ya kumi!

Kwa x kuwa zaidi ya kumi bado anaweza kukokotoa idadi ya wanaume kama y haijazidi kumi, ili kuharibu mlinganyo kabisa jifanye watoto wa kike ni zaidi ya kumi na wakiume pia ni zaidi ya kumi!

Lakini pia kama jamaa anajifanya mjanja wakusoma akili za watu, mwambie asome na jibu lako pia!

Ujanja huu unafanyaje kazi?
Kiufupi katika huu mlinganyo

(x * 2 + 3 )* 5 + y - 15

Jamaa ni anatuzungusha kimahesabu tu, atakuambia jumlisha hiki, zidisha na kile, kisha kuna hatua atakuambia utoe vile vyote ulivyovizidisha au kujumlisha kwa hiyo inakua kama haujafanya chochote. Ndio maana mwisho anakuambia utoe 15, ili kuondoa 15 aliyoizalisha wakati wa kujumlisha 3 kisha kuzidisha na 5. Hebu tuufungue mlinganyo wote tuone

2x + 15 + y - 15

Hapa utaona anaiondoa ile 15 iliyozalishwa.

Ili kumchanganya mtu zaidi idadi za hatua zinakua nyingi ili mtu ashangazwe zaidi jamaa anapopatia jibu

Natengenezaje mlinganyo wangu?
Katika ujanja huu, mbinu kubwa ipo kwenye kutenganisha x na y kwenye makumi na mamoja, kwa hiyo mlinganyo wowote utakao uwaza hakikisha unarahisishika kuwa 10x + y. Maana za x na y unaweza kuzigeuza ukipenda, yaani x kuwa watoto wa kike na y wakiume.

Mifano ya milinganyo tofauti
( x*2 + 4 ) * 5 + y - 20
(( x3 + 2 ) * 10 + y3 - 20 ) / 3

Ujanja wa variable moja

Ujanja huu ni rahisi sana kuutunga. Katika fungu hili kuna namna mbili za milinganyo.
Namna ya kwanza unaweza kutengeneza mlinganyo ambao mwisho utamuuliza jibu ni ngapi. Na namna ya pili hautauliza jibu, wewe ndio utamtajia jibu lake baada ya mahesabu yote.

Namna ya kwanza: kuuliza jibu, kisha kutaja namba iliyofikiriwa
Tuchukulie mfano wa mlinganyo ufuatao
(x * 2 + 3 )* 5 - 15

Ambao tukirahisisha unakua
10x

Sasa kama tumeuliza jibu akataja ni 20, tutaigawanya 20 kwa 10 na kupata 2, hivyo tutamwambia namba iliyofikiriwa ni 2.

Mlinganyo unaweza kuwa unavyotaka ili mradi iwe rahisi kukokotoa x.

Namna ya pili: kutaja jibu moja kwa moja
Katika namna hii hatutaji namba iliyofikiriwa bali tunataja jibu la mwisho baada hatua zote kufanyika.
Katika milinganyo hii mbinu kubwa ni kucancel x kihesabu

Kwa mfano
(( x*2 + 10 ) - 4 ) / 2 - x

Ukirahisisha unakua
(2x + 10 - 4 ) / 2 - x = x + 3 - x = 3

Hapa utaona pamoja nakuzunguka kote, ukirahisisha mlinganyo jibu ni 3, haijalishi umefikiria namba gani.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...