Je una application ambayo inalisten kwenye port fulani na ungependa port isiwepo kwenye url ya hiyo application? Au una nodejs application inayorun kwenye port fulani? kiufupi unataka kubadili https://domain.com:8080/api kuwa https://domain.com/app1/api Katika somo hili tutajifunza namna ya kutumia nginx kama proxy. nginx ni web server maarufu sana, pamoja na umaarufu wake kama web server pia inaweza kutumika kama proxy au load balancer. 1. Basic setup server { listen 80; server_name domain.com www.domain.com; ... location /app1/api { proxy_pass http://localhost:8080; } ... } location /app1/api inaiambia nginx ifananishe path ya url kama imematch /app1/api basi ipitishe request zote kwenda kwenye upstream server iliyopo kwenye url http://localhost:8080. Hii URL inaweza kuwa server nyigine kutegemea application yako ipo wapi. Kwa server nyingine URL inaweza kuwa proxy_pass http://IP_ADDRESS:PORT; 2. HTTP Headers Kwa ka...
Control Structures katika C Katika somo hili tutajifunza vitu au vipande mbali mbali vinavyounda programu kwa ujumla. Kwa kawaida kompyuta inarun programu mstari mmoja baada ya mwingine kwa kufuatana upi umeanza na upi unafuata. Mstari wa kwanza unarun, kisha unaofuatia na kuendelea hadi mwisho wa programu. Ili kuwepo na wigo mpana wa kuunda programu inabidi tuweze kuhama au kuruka mstari mmoja kwenda mwingine kutegemeana na masharti. Hii huwa inaitwa "Transfer of Control". Hapo awali programmers walikuwa wanatumia goto statement, ambayo inaiambia programu iende kwenye mstari fulani kutegemea na sharti fulani. Ilikuja kugundulika kuwa hii goto statement ilisababisha ugumu mkubwa kwa watengenezaji wa programu kwani kwenye programu kubwa ya kiuhalisia unakuta kuna goto nyingi ambapo inafika kipindi inakua vigumu kujua au kukumbuka statement fulani ilikua kwa sababu gani. Katika utafiti uliofanywa na Bohm na Jacopini walifanikiwa kuonesha kuwa programu zinaweza kutenge...