Je unataka kusoma nchi za nje kwa scholarship? Katika makala hii tutaona njia mbali mbali za kutafuta scholarship. Mtandaoni Dunia imebadilika tunaweza kupata taarifa mbali mbali kwenye simu zetu za viganjani au kompyuta, vile vile taarifa za scholarship zinapatikana kwa wingi kwenye mtandao. Unaweza kutumia google.com kutafuta scholarship zozote unazotaka kwa nchi yoyote duniani. Muhimu ni kuwa specific na unachotaka. Kwa mfano kama unataka kwenda USA ni vizuri ukasearch “scholarships in USA for international students” na sio “scholarships”. Kama matokea yatakayokuja ni machache unaweza kupunguza uspecific wako kidogo. Kwa ufupi inabidi uwe mjanja wa kutumia google. Vile vile vyuo vikuu vingine huwa vinatoa scholarship kwa wanafunzi wakigeni, hivyo ni vizuri kutembelea tovuti za vyuo hivyo. Mfano vyuo vikuu vingi vya marekani huwa vinatoa scholarships kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya SAT (kwa undergraduate). Pia kuna tovuti mbali mbali zinazoweka listi ya s...