Skip to main content

Posts

Jinsi ya kutumia nginx kama proxy au load balancer

Je una application ambayo inalisten kwenye port fulani na ungependa port isiwepo kwenye url ya hiyo application? Au una nodejs application inayorun kwenye port fulani? kiufupi unataka kubadili https://domain.com:8080/api kuwa https://domain.com/app1/api Katika somo hili tutajifunza namna ya kutumia nginx kama proxy. nginx ni web server maarufu sana, pamoja na umaarufu wake kama web server pia inaweza kutumika kama proxy au load balancer. 1. Basic setup server { listen 80; server_name domain.com www.domain.com; ... location /app1/api { proxy_pass http://localhost:8080; } ... } location /app1/api inaiambia nginx ifananishe path ya url kama imematch /app1/api basi ipitishe request zote kwenda kwenye upstream server iliyopo kwenye url http://localhost:8080. Hii URL inaweza kuwa server nyigine kutegemea application yako ipo wapi. Kwa server nyingine URL inaweza kuwa proxy_pass http://IP_ADDRESS:PORT; 2. HTTP Headers Kwa ka...

Control structures katika C

Control Structures katika C Katika somo hili tutajifunza vitu au vipande mbali mbali vinavyounda programu kwa ujumla. Kwa kawaida kompyuta inarun programu mstari mmoja baada ya mwingine kwa kufuatana upi umeanza na upi unafuata. Mstari wa kwanza unarun, kisha unaofuatia na kuendelea hadi mwisho wa programu. Ili kuwepo na wigo mpana wa kuunda programu inabidi tuweze kuhama au kuruka mstari mmoja kwenda mwingine kutegemeana na masharti. Hii huwa inaitwa "Transfer of Control". Hapo awali programmers walikuwa wanatumia goto statement, ambayo inaiambia programu iende kwenye mstari fulani kutegemea na sharti fulani. Ilikuja kugundulika kuwa hii goto statement ilisababisha ugumu mkubwa kwa watengenezaji wa programu kwani kwenye programu kubwa ya kiuhalisia unakuta kuna goto nyingi ambapo inafika kipindi inakua vigumu kujua au kukumbuka statement fulani ilikua kwa sababu gani. Katika utafiti uliofanywa na Bohm na Jacopini walifanikiwa kuonesha kuwa programu zinaweza kutenge...

Jinsi ya kuangalia faini za makosa ya barabarani Tanzania

Je ungependa kufahamu namna ya kucheck kama gari yako inadaiwa au haidaiwi? Unaweza kupata taarifa hizi kwa kutumia mtandao kwa wale wenye simu za internet, vile vile unaweza kutumia simu ya kawaida isiyo na internet. Kwa njia ya mtandao Kwa kutumia mtandao tembelea link ifuatayo. http://tms.tpf.go.tz Ukurasa ukifunguka ingiza namba ya gari lako, hapo utaona faini zilizopo katika gari lako. Pia unaweza kuchagua kuingiza namba ya leseni, ili upate faini zilizoandikwa katika leseni yako. Kwa njia ya simu Kwa kutumia simu ya kawaida piga *152*75#  , kisha fuata maelekezo, ukishamaliza utatumiwa ujumbe mfupi wenye taarifa za faini.

Fahamu file aina ya zip na jinsi ya kulitumia

Umewahi kudownload file kwenye internet na kukuta hilo file ni zip na ukashindwa kulifungua? Au umepokea barua pepe ndani yake kumeambatanishwa na file la zip? Au una file kubwa la game au software nyingine unataka kuliweka kwenye DVD lakini halitoshi kwenye hiyo DVD? Katika makala hii tutaangalia kwa undani file la zip (kifurushi) na matumizi yake mbali mbali. File la zip ni nini? File la zip ni file ambalo linakusanya mafile mengine na kuyaweka katika file moja. Hii huwa inarahisa kazi tofauti mfano kutuma barua pepe, badala ya kutuma mafile 10 yaliyomo kwenye folder moja, unaweza kutengeneza zip file moja na kulituma. Pia zip file husaidia kupunguza size ya file. Mfano mzuri wa mafile ambayo hupungua size maradufu ni mafile ya maandishi(text). Mafile ya picha, sauti au video mara nyingi hayapungui size sana kwa sababu aina za hayo mafile tayari yalishajaribu kuyapunguza size. Naandaa vipi file la zip? Ni rahisi sana kutengeneza file la zip, kwani utengenezaji wa file la zi...

Matokeo ya kidato cha sita 2018 haya hapa!

Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018. BONYEZA HAPA KWENDA KWENYE MATOKEO! Akizungumza na vyombo vya habari Dkt. Msonde alisema ufaulu kwa ujumla umeongezeka kutoka asilimia 96.06 ya mwaka jana na kuwa asilimia 97.12 mwaka huu, ingawa ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka kulinganisha na masomo ya biashara na sanaa. Vile vile ufaulu katika madaraja ya I, II na III umeongezeka ukilinganisha na mwaka jana. Ufaulu wa madaraja haya umeongezeka kwa asilimia 1.80 kutoka asilimia 93.72 ya mwaka jana na kuwa asilimia 95.52 kwa mwaka huu. Shule kumi zilizofaulu vizuri kitaifa ni kama ifuatavyo Na Shule Idadi ya watahiniwa Mkoa 1 Kibaha 121 Pwani 2 Kisimiri 68 Arusha 3 Kemebos 32 Kagera 4 Mzumbe 121 Morogoro 5 Feza Boys 93 Dar es salaam 6 Marian Boys 78 Pwani 7 Ahmes 76 Pwani 8 St Mary's Mazinde Juu 189 Tanga 9 Marian Girls 71 Pwani 10 Feza Girls 75 Dar es salaam BONY...

Jifunze kutype kwenye kompyuta bila kuangalia keyboard

Je unataka kuongeza ufanisi katika kazi zako za kompyuta? Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutype(kuandika) haraka haraka katika keyboard ya kompyuta bila kuangalia. Kutype haraka katika kompyuta ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza japo wengi hudhani wataalamu wa kompyuta ndio wanafanya mambo hayo. Ni ujuzi rahisi sana kama mtu ni mwenye bidii hata ndani ya mwezi unaweza kujifunza. Kuna usemi usemao mti wa kudakia samaki (fishing rod) ni mwendelezo wa mkono wa mvuvi, kwa maana mvuvi mahiri anaweza kuhisi pindi samaki anapokuwa maaneo ya mti wake. Kama fishing rod ilivyo kwa mvuvi, keyboard ya kompyuta inabidi iwe mwendelezo wa vidole vyako ili uwe mtumiaji wa kompyuta mzuri. Katika keyboard ya kompyuta kila kidole kina sehemu yake na kina sehemu kinaweza kwenda. Kujifunza kutype ni kujifunza namna ya kutumia vidole vyako inavyotakiwa. Katika kutype jambo kubwa la kuepuka ni kuinua mkono ili kufuata kitufe fulani, bila shaka kuna wakati utahitaji kuinua mkono lakini hii...

Ujue ujanja wa “Fikiria Namba” kihesabu

Je unataka kuwa mjanja wa kusoma fikra za watu? Hapa tutaona namna ya kutumia hesabu kiujanja zaidi. Ni jambo ambalo watu wengi hawalijui hivyo kuwa rahisi kudanganywa na watu wanaojifanya wanasoma akili za watu. Ujanja wa variable mbili( Ujanja wa 10x + y) Katika mfano huu ili usiwe kihesabu zaidi na rahisi kwa kila mtu kuelewa ntatoa mfano wa namna inavyotumika kisha ntawaonyesha kihesabu wewe unavyoweza kufanya na pia kutengeneza mlinganyo wako mwenyewe. Mfano mtu anaweza kuja akakuambia leo ntakutajia kwenu mpo wangapi, watoto wa kiume ni wangapi na wakike ni wangapi. Ataanza kukuambia chukua idadi ya watoto wa kiume zidisha kwa mbili, kisha jibu jumlisha na tatu, jibu lake zidisha na tano, kisha jumlisha idadi ya watoto wa kike, kisha toa 15 katika jibu. Baada ya hapo atakuuliza jibu ni ngapi. Ukimpa jibu tuseme 23, atakuambia mpo watoto watano, wakiume wawili na wakike watatu. Hapo utaona jamaa bonge la superhero!! Ngoja tuone namna yakufanya huu ujanja kihesabu Tuchuk...

Scholarship za Japan

Je ungependa kwenda kusoma nchini Japan kwa scholarship? Katika makala hii tutazungumzia scholarship ijulikanayo kama Monbukagakusho(MEXT) yaani wizara ya elimu, utamaduni, michezo, sayansi na teknolojia ya Japan. Serikali ya japan huwa inatoa scholarship kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao kwenda kusoma nchini Japan.  Scholarship hii ni maalumu kwa wanafunzi wanaofanya vizuri masomoni hivyo katika hatua za kuapply huwa kuna mchujo unafanyika wa wanafunzi. Mchujo huu huwa ni mtihani unaofanywa katika ubalozi wa japan katika nchi husika. Mtihani huwa na masomo ya kiingereza, hesabu nk (kwa undergraduate)  Application ya scholarship hii ni moja kwa moja kupitia ubalozi wa Japan uliopo nchini kwako.  Mara nyingi scholarship hii ipo kila mwaka, ingawa kwa baadhi ya miaka nchi kadhaa huwa hazina hii scholarship. Ili kuwa na uhakika juu ya scholarship hii ni vizuri kutembelea ubalozi wa Japan na kuiulizia.

Jinsi ya kutafuta scholarship

Je unataka kusoma nchi za nje kwa scholarship? Katika makala hii tutaona njia mbali mbali za kutafuta scholarship. Mtandaoni Dunia imebadilika tunaweza kupata taarifa mbali mbali kwenye simu zetu za viganjani au kompyuta, vile vile taarifa za scholarship zinapatikana kwa wingi kwenye mtandao. Unaweza kutumia google.com kutafuta scholarship zozote unazotaka kwa nchi yoyote duniani. Muhimu ni kuwa specific na unachotaka. Kwa mfano kama unataka kwenda USA ni vizuri ukasearch “scholarships in USA for international students” na sio “scholarships”. Kama matokea yatakayokuja ni machache unaweza kupunguza uspecific wako kidogo. Kwa ufupi inabidi uwe mjanja wa kutumia google. Vile vile vyuo vikuu vingine huwa vinatoa scholarship kwa wanafunzi wakigeni, hivyo ni vizuri kutembelea tovuti za vyuo hivyo. Mfano vyuo vikuu vingi vya marekani huwa vinatoa scholarships kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya SAT (kwa undergraduate). Pia kuna tovuti mbali mbali zinazoweka listi ya s...

Scholarship za uturuki

Je unataka kwenda kusoma nchi za nje hususani uturuki? Makala hii itakuonesha scholarship mbali mbali zinazopatikana nchini uturuki katika ngazi tofauti za elimu, kuanzia High school, undergraduate na kuendelea. Zifuatazo ni scholarship tofauti tofauti za uturuki na utaratibu wake wa kuapply. Scholarship za serikali ya uturuki Serikali ya uturuki huwa inatoa scholarship kwa wanafunzi wa nchi mbali mbali kwenda kusoma nchini uturuki katika ngazi tofauti za elimu kuanzia undergraduate mpaka PHD. Pia scholarship hii ni kwa ajili ya masomo yote sio udaktari na uhandisi pekee, kwa hiyo watu wa vitengo vingine wanaweza kuapply kama wahasibu na kadhalika. Application zinafanyika mtandaoni kupitia link ifuatayo. https://www.turkiyeburslari.gov.tr/en/english-home/ Scholarship za IDB Scholarship za IDB yani Islamic Development Bank zinatolewa kwa ajili ya wanafunzi wa ngazi mbali mbali kuanzia undergraduate na kuendelea. Scholarship hizi ni kwa ajili ya waislamu. Utaratibu wa kuapply ni ...

Kuwa mwalimu wa kiingereza na TEFL

Je unataka kuwa mwalimu wa kiingereza anayetambulika katika nchi nyingi? Au wewe si mwalimu lakini ni mjuzi wa kiingereza na unataka kupata kazi ya ualimu kirahisi? Katika makala hii tutaona mtihani wa TEFL na umuhimu wake. TEFL kwa kirefu ni Teaching English as a Foreign Language. TEFL ni kwa ajili ya kifundisha kiingereza kwa wanafunzi ambao lugha yao ya asili sio kiingereza. Kwa hiyo TEFL inatumika zaidi katika nchi ambazo haziongei kiingereza kama Spain, Uturuki, China na kadhalika. Pia TEFL hutumika katika nchi zinazoongea kiingereza ili kufundishia kiingereza wahamiaji katika nchi hizo. Huu ni mtihani ambao ukishafaulu na kupata cheti utakuwezesha kufundisha kiingereza katika shule mbali mbali duniani kote. Ni mtihani wa kimataifa, kwa hiyo unatambulika nchi nyingi. Vile vile vituo vya kufanyia mtihani huwa vinasaidia kupata kazi katika nchi mbalimbali. Kwa mfano seriousteachers.com wao huwa wanapata kazi nyingi kutoka kwa waajiri wanaohitaji walimu wa TEFL, nao huzisambaz...

Algorithm na Pseudocode

Je unataka kujua mbinu ya kuandika programu iliyo bora? unataka kuwa tofauti na programmer wengine wa kawaida? Algorithm ni nini? Algorithm ni MFULULIZO wa hatua zilizo katika MPANGILIO MAALUMU zinazofanikisha kazi fulani. Mfano unaweza kuwa na kazi ya kuhesabu watu, au kazi ya kuamka asubuhi au kazi ya kula chakula au kazi na kutengeneza juisi. Katika kazi ya kula chakula, algorithm inaweza kuwa hivi Pika chakula Andaa chakula mezani Nawa mikono Kula Na katika kazi ya kutengeneza juisi, mfano juisi ya nanasi, algorithm inaweza kuwa hivi Osha tunda Menya nanasi Kata vipande vidogo vidogo Weka vipande katika blenda Ongeza maji na sukari Saga mchanganyiko katika blenda Mpangilio katika Algorithm Katika hatua hizi za algorithm utagundua kwamba tukigeuza hatua tu, tunaweza kuharibu hiyo kazi. Kwa mfano, katika kazi ya kutengeneza juisi ya nanasi, tukihamisha hatua ya kwanza kuwa ya mwisho, tutakuwa tumetengeneza juisi yenye uchafu katika maganda yake. Hivyo basi wa...

Maamuzi katika programu - Alama za usawa na uhusiano

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia alama zingine za hesabu katika programu zetu. Tutajifunza alama za aina mbili yaani alama za usawa (Equality Operators) na alama za uhusiano (Relational Operators). Alama hizi ni muhimu kufahamu matumizi yake kwani katika alama tutakazozitumia sana katika programu zetu. Kwa mfano tunataka kutengeneza programu itakayopanga matokeo ya wanafunzi katika grade A, B, C na kuendelea. Ili kujua kama grade ya mwanafunzi ni A, itabidi tucheki kama grade ni kubwa kuliko au sawa na 80 ( grade >= 80). 80 tumeitumia kama mfano tu, bila shaka utatumia namna grade zinavyopangwa katika level flani. Mfano mwingine, tunaweza kutaka kujua wanafunzi wote ambao hawajapata sifuri, katika programu hii tutacheki kama grade sio sawa na sifuri ( grade != 0 ). Jedwali lifuatalo linaonesha alama za usawa. Alama katika hesabu Alama katika C Mfano Maana = == x == y x ni sawa na y ≠ != x != y x sio sawa na y Jedwali ilifuatalo linaonesha ...

Arithmetic katika C

Ni kawaida katika programu kutaka kutumia mlinganyo(equation) au kanuni(formula) flani katika programu yako. Kwa mfano unaweza kuandika programu ya kukokotoa eneo la duara, katika programu hii itabidi uandike kanuni ya eneo la duara, hivyo ni muhimu kufahamu alama tofauti za hesabu zinavyoweza kuandikwa katika programu zetu za C. Jedwali lifuatalo linaonyesha alama katika C na katika aljebra Alama Aljebra C Kujumlisha a + b a + b Kutoa y - x y - x Kuzidisha ab a * b Kugawanya x / y au x ÷ y x / y Baki(Remainder) a mod b a % b Katika jedwali hili utagundua kwamba alama nyingi za kihesabu zinafanana na zile za C, isipokuwa alama mbili za kuzidisha na baki. Kuzidisha katika C kunawakilishwa na alama ya asterisk(*), katika hesabu tukiandika ab, inamaanisha a zidisha na b, lakini katika C tukiandika ab inamaanisha jina la variable ab, hivyo ili kuondoa mgongano wa maana, alama ya asterisk(*) hutumika. Alama ya asilimia(%) inawakilisha baki au salio ...

Programu rahisi ya C: kujumlisha namba mbili

Je unataka kujua namna ya kufanya mahesabu katika programu? Programu yetu ya sasa itaonyesha namna ya kujumlisha namba mbili ambazo mtumiaji atakuwa ameingiza kwa kuandika na keyboard yake. Kama tulivyojifunza hapo awali kuwa stdio.h ni “Standard Input/Output header”, ambalo ni file lenye functions zinazohusiana na input(kuingiza) au output kama vile printf, kwenye somo hili tutajifunza function mpya ya scanf. Kazi ya scanf ni kuchukua/kusoma alichoandika mtumiaji kwa keyboard na kukihifadhi katika kompyuta kwa matumizi ya baadae kwenye programu. Programu ifuatayo inaonyesha kujumlisha tarakimu mbili #include <stdio.h> /* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */ int main(void) { int namba1; /* namba ya kwanza itakayoingizwa */ int namba2; /* namba ya pili itakayoingizwa */ int jumla; /* variable itakayohifadhi jumla */ printf("Andika namba ya kwanza\n"); /* julisha kuwa namba inatakiwa kuingizwa */ scanf("%d"...

Programu rahisi ya C: kuandika maandishi kwenye screen

Je unataka kuona jinsi programu ya C inavyoandikwa? Katika somo hili tutajifunza machache katika C, kadri tunavyoendelea kujifunza ntaongeza vitu mbali mbali kidogo kidogo, ili na wewe uweze kutafuna uliyojifunza! 1. Kuandika maandishi kwenye screen Programu ifuatayo itakuonyesha namna ya kuandika maandishi kwenye screen #include <stdio.h> /* function main - Hapa ndipo programu inapoanzia kufanya kazi */ int main(void) { printf("Karibu C Programu!\n"); return 0; /* Programu imemalizika bila tatizo */ } /* Mwisho wa main */ Output Karibu C Programu! 1.0. #include <stdio.h> Hii inaiambia C Preprocessor kuweka yaliyomo katika file la stdio.h kwenye hii programu. File la stdio.h yaani standard input/output header lina maelezo ambayo yanasaidia COMPILER kucompile programu yako kama umetumia function zilizomo humo. Kwa mfano printf ni moja ya function ambazo zipo kwenye stdio.h, kuna zingine nyingi tutaendelea kujifunza. function ni kipan...

Jinsi ya kujifunza lugha ya kuprogramu ya C

Je unataka kuwa mtaalamu wa kutengeneza programu za kompyuta? unataka kufahamu njia ya kutimiza lengo lako kirahisi? Waswahili wanasema "Mtaka cha uvunguni sharti ainame" basi ndivyo hivyo hivyo ili kuwa mtaalamu wa kuprogramu inabidi uwe unaandika programu. Ujuzi wowote unaushika vizuri zaidi ukiwa ni mtendaji. Utajifunza mengi sana kwa kuandika programu zaidi ya kusoma C kwenye vitabu na mtandaoni. Hivyo weka bidii kufanya mazoezi tofauti tofauti ya kuprogramu iwe kwenye vitabu au kutengeneza programu ya suluhisho ya matatizo uliyoyaona mtaani, kwenye biashara au sehemu nyingine. Pia wakati unafanya mazoezi haya jitahidi kufuata miongozo ya kuandika programu nzuri yaani GOOD PROGRAMMING GUIDELINES. Kwenye programu zako hakikisha zinasomeka vizuri kwa maana nafasi kati ya maneno au mistari iwe ya kutosha. Pia jitahidi kuweka maoni (COMMENTS) ili iwe rahisi wewe kuelewa au mtu mwingine kuelewa programu yako. Ni kawaida kwa programmer kusahau sehemu flani ya programu yake ...

Historia fupi ya C

Je unataka kujua C ilitokea wapi? na kipindi gani? Lugha ya kuandikia programu za kompyuta ya C ilianzishwa mnamo mwaka 1970 na mbunifu wake Dennis Ritchie. Aliita C kwa sababu kipindi hicho alikuwa akitumia lugha iitwayo B katika kazi zake, hivyo C ilifuata baada ya B. Mbunifu wa C alichukua mazuri ya B na kuyaweka kwenye C, vile vile akaongeza maboresho ambayo kwenye B yalikuwa ni vikwazo. C ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kutengenezea OPERATING SYSTEMS kwa kipindi hicho UNIX. Hata mbunifu wa B alipotengeneza B alianza kuitumia kuandikia UNIX OPERATING SYSTEM. C ilikuwa rahisi sana kutumia, hivyo ikaanza kutumika katika matumizi mengine nje ya OPERATING SYSTEMS. Haikuchukua muda mrefu C ikawa lugha maarufu sana duniani kote ya kuandikia programu za kompyuta. Umaarufu wa C ulichangiwa na urahisi wake, ambapo programmer aliweza kufanya chochote alichotaka kirahisi bila kupitia vikwazo vingi. Vile vile programu za kubadilisha C kwenda kwenye MACHINE CODE yaani COMPILER zilipatik...

Jinsi kuprogramu kompyuta kunavyofanya kazi

Je unajiuliza ni namna gani kuprogramu kompyuta kunavyofanya kazi? Leo tutaingia ndani ya kompyuta na kuelewa namna inavyofanya kazi. MACHINE CODE NA ASSEMBLY LANGUAGE Kwanza kabisa inabidi tuelewe kwamba kompyuta inaelewa sifuri na moja au ON na OFF pekee, ambazo huitwa BINARY DIGITS. Mfululizo wa hizi binary digits kwa namna ambayo kompyuta inaelewa huitwa MACHINE CODE yaani lugha ya mashine. Kwa mfano, Kujumlisha kunaweza kuwakilishwa na 1010 kutoa kukawakilishwa na 1011 ufuatao ni mfano wa programu katika MACHINE CODE: 0011 1111 1010 0111 1011 0110 ... na kuendelea sasa huu mfululizo wa haya maelezo (INSTRUCTIONS) ndio unaounda programu ya kompyuta. Lakini kuna tatizo moja ni vigumu sana kuandika programu kwa machine code, yaani kwa sifuri na moja. kutokana na ugumu huu lugha nyingine ambayo ni rahisi kwa mwanadamu iliundwa ambayo ni ASSEMBLY LANGUAGE. Lugha hii inatumia maneno kuwakilisha zile zile binary digits. kwa hivyo badala ya programmer kuandika 1010 anaandika A...